Picha ya ajabu ya Gerard Quenum


Nini sawa kati ya wasanii hawa wawili wa Benin wenye acrylic kwenye canvas Gérard Quenum? Kwanza kaaka ya rangi iliyozuiliwa (mchoraji anapendelea kutumia nyeusi na nyeupe na ikiwezekana rangi za msingi). Lakini pia miundo iliyoonyeshwa kama picha nyeusi za vinyago zilizopunguzwa kuwa vivuli. Na mwisho kabisa, maudhui ayapendayo msanii, ile ya usafirishaji wa umma inayoashiria wendo na mwendo. Katika kazi hizi mbili zilizoundwa mwaka wa 2013, Gérard Quenum anazizimbua zote mbili; kukaa kwake London na Taxi Londres kama tu Benin na bara kubwa ka Afrika na Taxi brousse. Teksi za kichakani ndizo zinazoelezea vyema hali ya usafirishaji barani Afrika. Licha ya saizi yao ndogo, huwa zinabeba vitu vingi zaidi ambazo hujaza paa zao.

Gérard Quenum aliwakilisha picha hii na nyumba kubwa ya ndege iliyomo na ndege.

Mhusika aliye nje ya teksi anasimamia kwa uzito mkuu, halaiki, inayohusishwa kwa sana na furaha inayopatikana kwenye stendi za basi za Afrika.

Picha ya ajabu ya Samuel Fosso


Wahusika wenye rangi nyingi na maarufu pekee! Mharamia? Mbepari? Mlinda maisha, Mbaharia, Nyota wa rock, Chifu wa kiafrika? Na bado mada huwa ile ile: mpigaji picha achukuaye jukwaa kupitia picha zake binafsi, ambapo yeye hutokea akiwa amevalia nguo za jinsia isiyo yake, iliyo na wahusika wenye mifano ya kejeli na wa hadithi za kitambo. Picha hizi kumi zinauunda mifululizo ya TATI iliyoundwa mwaka wa 1997, katika tukio la makumbusho ya hamsini ya maduka mfululizo maarufu yaliyoko katika mazingira ya kijirani ya Barbès, Paris. Mifululizo ya TATI, zaidi ya mbishi, ina mwelekeo muhimu: Samuel Fosso anatumia picha yake na kujificha kwake kuagiza za kawaida za Magharibi ama siasa.

Mcamerooni huyu aliyesanikishwa kwa miaka mingi kule Bangui, Jamhuri ya Afrika ya Kati, Samuel Fosso anaunda daima, tena kwa kupitia jinsia ambako ana umahiri wa hali ya juu: picha ya mtu mwenyewe.

Picha ya ajabu ya Bruce Clarke


Tuelekee kugundua kazi mbili za Sanaa kwenye maudhui ya Ndondi: L’impensable, 2005 na The Game Begins, 2011. Karibia na utatofautisha mbinu kamili, Bruce Clarke, msanii wa Uiengereza, mwenye asili ya Afrika Kusini. Yeye huunganisha picha na Sanaa unganishi yaani collage, maneno na picha, kwa kuchezea maongezo na yaletayo uwazi. Mwanaharakati aliyejitolea, Bruce Clarke anazungumzia spoti ambayo historia yake imeunganishika kwa undani na kupigania haki za kiraia. Nchini Marekani, ndondi kati ya weupe na weusi ilikuwa imekatazwa. Mwaka wa 1910, Jack Johnson, bingwa wa dunia wa ndondi na mweusi wa kwanza, hakuruhusiwa kutetea ubingwa wake. Mapigano ya utambuzi wa ubingwa wake yanaweza kuchukuliwa kama msingi wa kupigania usawa kati ya weusi na weupe. Baada ya kuruhusiwa kwake kupigana tena, matangazo ya ushindi wake yalisababisha vita vya kiubaguzi wa rangi nchini huko. Ndondi ikawa katika nusu ya pili ya karne ya ishirini, kwa wakati mwingine, njia pekee ya kuboresha hali ya kijamii. Bruce Clarke anazungumzia ndondi kama sitiari ya mapigano ya kisasa ya kijamii.

Picha ya ajabu ya Frédéric Bruly Bouabré


Uko mbele ya Shujaa Bekora, mifululizo ya michoro midogo 12 ya Frederic Bruly Bouabré, msanii mwenye asili ya Cote d’ivoire aliyeaga Dunia mwaka wa 2014. Unapokaribia sana, unaweza ona kuwa wanaunganisha michoro na maandishi na yanatengenezwa kwenye bodi ya kadi, kwenye karatasi ya penseli, michoro karatasi na wino.

Mfululizo huo unaeleza hadithi kuhusu mwindaji kwa jina Bekora ambaye, wakati wa sherehe ya uwindaji, alikutana na GBLI, joka la chatu na kumkombolea maisha yake. Kwa shukrani zake, Gbli alipendekeza kumpa kila kitu alichotaka. Bekora akasema kutokufa. Gbli basi akamuonyesha mmea wa hirizi na desturi ya kufuata unapoitumia. Kijijini, Bekora alimwambia mkewe hadithi ile ambaye alimwambia afanye desturi ile alpokuwa analala, akifuata maagizo ya joka lile. Baada ya masaa machache, yule mwanamke akagunduwa kuwa mumewe kakuwa mawe. Ndio asili ya msemo: "Atafutaye kutokufa huwa mawe."

Michoro kumi na miwili ya shujaa huyu, yanayoshirikishwa na maelfu ya mengine yaliyotengenezwa na Frédéric Bruly Bouabré yanatengeneza kazi ya sanaa iitwayo “Connaissance du monde” kampuni ya kiensaiklopidia na universal ambazo msanii huyu aliziendelelea kwa nusu karne.

Picha ya ajabu ya Cyprien Tokoudagba


Tumgundue Cyprien Tokoudagba! Kazi yake inalingana sana na historia ya kitamaduni na kidhehebu ya Ufalme wa Dahomey. Je, unaona nini? Mbogo? Tunda? Naam lakini ni mengi zaidi ya hayo. Amejikita sana kwenye ulingo wa kugeuza imani na historia katika michoro yake kwa kutumia acrylic, ndizo nembo za wafalme wa Dahomey zilizowakilishwa na Cyprien Tokoudagba, Msanii wa Benin aliyeaga dunia mwaka wa 2012. Mbogo, aliyetengenezwa mwaka wa 2005, ndiye nembo ya mfalme Guézo. Mnyama mwenye nguvu, kumaanisha hakuna kitakachomzuia mfalme katika kutekeleza mipango yake. Chini ya mbogo huyu, tunaweza tofautisha mota, inayoashiria jiji la Abomey, jiji kuu la ufalme ule. Tukiangazia tunda lile lililochorwa mwaka wa 2006, ndilo nembo ya mfalme Agonglo. Katika lugha ya kinyumbani, tunda la palmyra limeitwa Agon. Ishara hiyo inaashiria msemo wa "Radi ilipiga mnazi, lakini palmyra licha ya saizi yake kubwa, iliponyoka." Hii ni ishara ya moja kwa moja ya mfalme kuhepa mitego na kuzishinda changamoto za kutawala.

Picha ya ajabu ya George Lilanga


George Lilanga ni msanii wa Tanzania, aliyeaga dunia mwaka wa 2005. Michoro yake yenye rangi zinazong’aa zilizowekwa kwenye maeneo yaliyonyooka zinaonyesha asili bora za tamaduni ile ilipotoka, ya Makonde, watu wa kibantu-wanaoishi kwa sana kusini –mashariki mwa Tanzania na kaskazini mwa Mozambique. Anaelezea upya hadithi hizi za asilia kupitia paneli hizi nne zilizochorwa na na akriliki mnamo mwaka wa 1998. Inaonyesha ulimwengu wa viumbe nusu-binadamu, nusu-ajabu wenye vurugu na unaoungana. Uhuru unaovuma kwenye michoro hii, hata hivyo, zinahusika na ujenzi mkali ambapo miundo inafafanuliwa na muhtasari mweusi.

Picha ya ajabu ya Victor Omar Diop


Karibu kwenye Studio ya vanities. Haya mambo matatu ya kawaida ya 2011 ni mojawapo ya mifululizo za kwanza ya Victor Omar Diop, mpigaji picha Msenegali.

Utafahamu nambari za studio ya upigaji picha wa picha: picha zilizowekwa kwenye mkao kwa kuzingatia kwa kina, mavazi na mapambo, pamoja na chini zao. Zimeelezwa upya kwa urembo wa pop wa kisasa na zinayoonyesha manufaa ya Omar Diop Victor sio tu kwa upigaji picha, bali kwa muundo na mavazi. Kupitia michoro hii iliyowekwa kwenye mkao ya waigizaji wa onyesho la kitamaduni la miji ya Kiafrika, Ni kwa kweli upigaji picha wa kizazi anayekubaliana nayo: kizazi kinachofanya kazi kuhakikisha mseto wa maumbo ya kiafrika ya kisasa.

Picha ya ajabu ya Soly Cissé


Kazi hizi tatu za msanii msenegali Soly Cissé zilizochanganywa kwa mfululizo unaoitwa Bestiary, iliyotengenezwa kwa pastel na rangi ya acrylic kwenye karatasi mwaka wa 2009. Unaweza ona wahusika wa kushangaza na kuogofya wasiyo na miundo kamili. Kwa mchanganyiko usio wa kihesabu, Soly Cissé anasisitiza kwa sana dunia iliyoegemea usasa (inayoonyeshwa kupitia michoro na nambari za baa zilizotapakaa kwenye kazi yake) na dunia inayoshangaza, ile dunia ya ufalme wa wanyama. Kwa kuongeza idadi ya viumbe vyake, viumbe mseto, msanii ana maswali kuhusu hali ya binadamu inayobadilika.

Picha ya kiajabu ya Romuald Hazoumè


Tazama picha hizi mbili kutoka kwa msanii Mbenin Romuald Hazoumè. Rangi hizi na ugumu ulitoka wapi kwenye canvas? Msanii anatumia rangi asili: matope, kinyesi cha ngo’mbe, zambarau …Na hizi dalili zote? Mraba, duara, vituo, parafujo, mistari wimbi, mishale: maanake? Romuald Hazoumè, anaongeza michoro mbili, Lete-meji 1993 na The Queen ya 2006, dalili za Fa, Yoruba divination science. Inayoonyesha oni la kiulimwengu la Wayoruba, kila ishara ni ulimwengu mzima. Romuald Hazoumè anatumia kama kishikiliaji tamaduni ambapo anaelezea maswali kumhusu, kuhusu siku za usoni za Afrika, ama kuhusu ulimwengu unaobadilika. Msanii anaiita utamaduni huu, na kujifafanua kama "Ni", msanii anaayesafiri anayesambaza mila ya Wayoruba kwenye safari zake.

Picha ya kiajabu ya J.D.'Okhai Ojeikere


Uko mbele ya picha tatu za mfululizo wa mtindo wa nywele za mpigaji picha Mnaijeria-J.D.'Okhai Ojeikere. Msanii anafahamu umuhimu wa kazi ya upigaji picha kwa kuhifadhi utamaduni wake, inayopatikana kupitia mfululizo huu uliotengenezwa kuanzia 1968 hadi 1999, zaidi ya picha 1,000 zilizo na aina za mitindo ya nywele za wanawake Wanaijeria. Kwa hivyo, J.D.'Okhai Ojeikere anaunda kumbukumbu ya aina nyingi na mbali mbali za mitindo ya nywele, mhusika mwenye urembo na wa kuwekwa kwenye makumbusho. Afrika, kwa kweli, mtindo wa nywele sio tu kurembesha.Yeye pia ni muumbaji wa cheo cha kijamii cha mwanamke anayeivaa, na inashirikishwa na matukio tofauti ya maisha. Wanawake mara nyingi huuliza, bila kujitambulisha, umbo pande au uso. Fremu, inayoangazia nywele na kuonyesha kipengee cha muundo wake.

Mfululizo wa Mtindo wa nywele ni maharufu sana miongoni mwa kazi ya kibinafsi ambayo J.D.'Okhai Ojeikere anafanya mbali na kazi ya studio yake kama mtengenezaji picha, inamfanya aagize. Kwa msanii, aliyeaga dunia mwaka wa 2014, ni kazi iliyokusanywa: macho ya mpigaji picha inaunganisha msusi mwenye kipaji lakini pia chaguo la mteja aliyefanya ususi.

WakponSWA.html
WakponInfo.html
iWakponInfo.html

WAKPON – Jumba la makumbusho la kuta ni programu ya Shirika la Zinsou